Ndugu zangu Watanzania, kwa niaba ya Wananchi
wa Jimbo la Monduli na Familia yangu nachukua fursa hii kuwatakia ndugu
zetu Waislamu na Watanzania wote heri ya Sikukuu ya Eid EL-Fitri.
Ninawatakia Sikukuu yenye mafanikio, furaha na amani.
Kwa Ndugu zetu waislamu Sikuu ya Eid EL-Fitri ina mafundisho muhimu
sana ambapo kila Muislam mwenye uwezo anatakiwa kutoa sadaka iitwayo
'Zakaatul Fitri' hii ni baada ya kumaliza mfungo wa Ramadhani, Na kwa
wale ambao hawakufunga kutokana na sababu mbalimbali kama vile sababu za
kiafya unatakiwa kulisha masikini kwa chakula cha nafaka kipendwacho
na jamii husika. Aidha, Sikukuu hii huweka familia na jamii kusherekea
kwa pamoja.
Naomba nimalizie kwa kukiri kuwa natambua Sikuu ya
Eid EL-Fitri ni moja kati ya nguzo muhimu kwa dini ya Kiislaam, hivyo
basi niwaombeni mafunzo tuliyoyapata katika kipindi cha Swaumu
yaimarishe Upendo, Amani na kudumisha Utulivu tulionao kama Taifa.
Nawatakia Eid Mubaraak,
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.
Kupata taarifa zaidi za Mh. Edward Lowassa, na kuona maoni watu
mbalimbali kuhusu Elimu, Afya, Uchumi, Watu na Hali ya Makazi na Afya ya
Jamii ya Monduli tafadhali tembelea tovuti : http://www.elowassa.com/monduli_swahili.php
No comments:
Post a Comment