Waziri Mkuu Msataafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa Akihutubia wananchi katika Mkutano huo wa Hadhara
Mbunge
Lowassa akisikiliza majibu kwenda kwa wananchi yaliyokuwa yakitolewa
na Mkuu wa Kituo cha Polisi Mto wa Mbu, Mrakibu wa Polisi (SP) Morris
Okinda
Waziri
Mkuu Msataafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akisikiliza swali
kutoka kwa mwananchi Mkazi wa Mto wa Mbu, mkoani Arusha juu ya kero
mbalimbali zinazowakabili za kiusalama. Lowassa alifanya ziara hiyo jana
ya kuzungumza na wapiga kura wake.
Mbunge
wa Jimbo la Monduli Edward Lowassa akizungumza na kusalimia wananchi
katika eneo la Mto wa Mbu wakati wa mkutano wake wa hadhara.
--
WAZIRI
Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM),
kina tatizo la uongozi na utendaji lakini licha ya kasoro hizo ametaja
mambo matano yanayomfanya aendelee kuwa mwanachama wake.Mbunge huyo wa Monduli (CCM), alisema moja ya jambo hilo ni misingi yake ya awali likiwamo suala la kutetea wanyonge.
“Siku CCM inaacha kutetea wanyonge mimi si mmoja wao,” alisema juzi huko Mto wa Mbu, Monduli mkoani Arusha alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara.
“Pamoja na uzuri wake, muundo wa chama chetu ni mzuri sana, imani ya chama chetu ni nzuri sana, misingi inayoongoza chama chetu ni mizuri sana, lakini tuna tatizo la utendaji na uongozi ndani ya chama chetu,” alisema Lowassa na kuongeza:
“…Ama katika kufanya maamuzi, ama kufanya maamuzi yasiyo sahihi au kutochukua hatua kwa matatizo yanayowakabili wananchi kwa wakati muafaka.”
Lowassa alieleza kuwa matatizo hayo ndiyo yanayowafanya watu wakichukie chama hicho na kukiona kuwa ni kero kwao hivyo kutafuta mbadala wake.
Kauli hiyo ya Lowassa imekuja huku Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (Nec), ikitarajiwa kukutana Dodoma kuanzia wiki ijayo, pamoja na mambo mengine, kitajadili mustakabali wa kisiasa nchini.
Pia hii ni mara ya kwanza kwa Lowassa kukikosoa chama hicho kinachoongozwa na Rais Jakaya Kikwete anayeaminika kuwa mtu wake wa karibu.
“Misingi mitano inayonifanya niwe mwanachama wa CCM, moja ni kwamba ni chama kinachotetea wanyonge. Sababu nyingine ni umoja na mshikamano, msingi wa tatu ni kwamba raia wa kawaida analindwa katika kupata na kufaidi rasilimali za nchi dhidi ya matajiri na wawekaji wa nje. Msingi wa nne na tano ni mfumo unaowezesha watu kujisahihisha... “Ndani ya CCM kuna vikao, kuna taratibu za vikao, kuna kufukuzana, kuonyana, lakini kubwa, kuna haki za msingi za mwanachama za kupiga kura au kupigiwa kura.”Kwa Habari zaidi
No comments:
Post a Comment