Tuesday, 22 July 2014

Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa na Rais Mstaafu Wa Awamu Ya Pili Alhaj Hassan Mwinyi Waudhuria Sherehe za Kusimikwa Kwa Askofu Mkuu Mpya wa Jimbo la Ifakara Mkoani Morogoro.


Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili,Mh. Ally Hassan Mwinyi akihutubia kwenye Sherehe hizo.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akitoa salamu kwa wakristo waliofika kwenye Sherehe hizo jana,ambapo ameliomba Kanisa Katoliki kuisaidia serikali katika kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana.
Askofu Mkuu Mpya wa Jimbo la Ifakara,Muhashamu Salitaris Melchior Libena akiongoza ibada yake ya kwanza akiwa ni Askofu wa Jimbo Jipya la Ifakara mara baada ya kusimikwa jana
Askofu Mkuu Mpya wa Jimbo la Ifakara,Muhashamu Salitaris Melchior Libena akitoa baraka zake kwa Viongozi wa Serikali waliohudhulia Sherehe hizo za kusimikwa kwake jana.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Muadhama Polycarp Kardinali Pengo mara baada ya kumalizika kwa Sherehe ya Kuzindua Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki Ifakara na kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo hilo iliyofanyika jana Ifakara,Mkoani Morogoro.
Mh. Lowassa akibadirishana mawazo na Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea.
Mh. Lowassa akiwapungia mkono wakazi wa Ifakara.
Mh. Lowassa akizungumza na Mmoja wa wananchi wa Mji wa Ifakara.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akitoa salamu kwa wakristo waliofika kwenye Sherehe hizo jana,ambapo ameliomba Kanisa Katoliki kuisaidia serikali katika kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili,Mh. Ally Hassan Mwinyi akimpongeza Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero,kabla ya safari ya kuelekea kwenye Sherehe ya Kuzinduliwa kwa Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki Ifakara na kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo hilo.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera wakati wakielekea kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero jana.Watatu Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa akisalimiana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hadji Mponda kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera na Mzee Alli Hassan Mwinyi.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili,Mh. Ally Hassan Mwinyi (kushoto) na Mkewe Mama Sitti Mwinyi (katikati) wakiwa kwenye mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa (wa pili kulia) pamoja na Mkewe Mama Regina Lowassa (kulia) kabla ya kuanza safari ya kuelekea kwenye Sherehe ya Kuzinduliwa kwa Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki Ifakara na kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo hilo,Muhashamu Salitaris Melchior Libena iliyofanyika jana Ifakara,Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro.
Kwaya ya Watoto ikiimba katika ibada hiyo.
Waumini wa Kanisa Katoliki Ifakara wakiwa katika ibada hiyo.

No comments:

Post a Comment