Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba kutoka kundi
la 201,Thomas Magnus Mgoli amelazwa katika hospital ya mkoa Dodoma baada
ya kupigwa na vijana anaodai kuwa ni washabiki wa Chadema.Akizungumza
kitandani kwake Mgoli amesema alishambuliwa na vijana
hao jana usiku majira ya saa moja eneo la area D anakoishi.Amesema
vijana hao hukutana nao mara kwa mara anapokwenda dukani na huzungumzia
masuala ya bunge hilo, lakini hiyo jana walimshambulia kwa kumuambia
kuwa yeye ni CCM.Pichani Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mh.
Edward Lowassa akimjulia hali Mh Mgoli hospitalini hapo, wote wako
kamati namba 12. |
|
No comments:
Post a Comment