Waziri Mkuu wa zamani na mbunge wa
Monduli Mh Edward Lowassa amewanyooshea vidole viongozi wa
kimila(malaigwanani),viongozi wa vijiji na wale wa ccm wilayani humo,
kuwa wanalaumiwa kwa kushiriki katika uuzaji ardhi kinyume na sheria.
Akifungua semina ya siku mbili juu ya ardhi kwenye ukumbi wa hoteli
ya Emanyata mjini Monduli,Mh Lowassa amesema shutuma hizo zimekuwa
nyingi kwa kuuza utajiri(ardhi) na kununua umasikini.
Walikuja pale nyumbani kwangu wale watu wa maombezi(walokole), moja
ya mambo waliyoyalalamikia ni uzwaji wa ardhi.wakaniambia hivi Mh mbunge
hamuoni viongozi, vijiji an ccm pamoja na malaigwanan wanavyopokea
rushwa na kuuza ardhi?Wanavyowadhulumu wajane?" Alisema Lowassa na
kuongeza akaona kuna umuhimu wa kulijadili kwa kina suala,hilo.
Kutokana na hali hiyo Lowassa amewatahadharisha viongozi wa vijiji
kuhakikisha waiondoa kero hiyo, kabla ya uchaguzi ujayo wa serikali za
mitaa vinginevyo tatizo hilo litawagharimu.
Aidha Mh Lowassa ambaye yeye pamoja na mbunge wa Viti maalum Namelok
Sokoine ndiyo waliyoiandaa semina hiyo, amempongeza mbunge wa zamani wa
Monduli hayati Edward Moringe Sokoine, kwa kufanikisha makubaliano kati
ya wilaya na jeshi kuhusiana na matumizi ya ardhi.
Marehemu Sokoine alifanya jambo kubwa sana kwa kufikia makubaliano
yale na faida yake kwetu sisi wana Monduli ni kubwa kimejengwa Hapa Chuo
kikubwa cha kijeshi(TMA), na tulikubaliana tusilipwe fidia na jeshi ili
tuwe na haki kwa mifugo yetu kuingia eneo lile,lakini kuna watu
wameipeleka halmashauri mahakamani kupinga" alisema na kuonya kuwa"
tutapambana kuhakikisha tunashinda! tumekuwa na mahusiano mazuri na
jeshi na tunataka mahusiano hayo yaendelee".
Naye mbunge wa viti maalum Nameloki Sokoine alisema kuwa madhumuni ya
kuandaa semina hiyo ni kutoa dira itakayofafanua nini kifanyike kuondoa
tatizo hilo la uuzaji holela wa ardhi.
Amesema mifugo na binaadamu wamekuwa wakiongezeka lakini ardhi ni ile
ile kwa hivyo bila ya kuwepo kwa dira na mipango thabiti hali itakuwa
mbaya.
Aidha alitoa changamoto kwa mbunge wa Monduli Mh Lowassa kusaidia
kupatikana kwa wawekezaji wa viwanda vya maziwa, ngozi na nyama wilayani
Monduli.
Ningependa kumuomba Mh mbunge najua hili analiweza atusaidie watu wa
Monduli tupate wawekezaji wa viwanda vya ngozi, maziwa na nyama,tukiwa
na viwanda hivi itasaidia wafugaji kuachana na ufugaji wa kimila wa
ng'ombe wengi an badala yake kuwa na ng'ombe wachache wa kisasa wenye
tija" alisema Namelok na kushangiliwa.
No comments:
Post a Comment