Waziri mkuu wa zamani na mbunge wa Monduli Mh Edward
Lowassa(kulia)akiwakaribisha mawaziri wa zamani wa Kenya William ole
Ntimama(tai nyekundu) na John Keen(kushoto) nyumbani kwake Monduli.
Wanasiasa hao wakongwe na wenye ushawishi mkubwa katika eneo la Maasai
Land nchini Kenya walimtembelea Mh Lowassa ambaye ni Laigwanan mkuu wa
wamasai wote Afrika mashariki, na kujadiliana naye masuala mbalimbali
lakini zaidi ni juu ya suala la ardhi ambalo limekuwa tatizo kubwa kwa
jamii ya wamasai.Wazee hao wanatarajiwa
kuudhuria semina maalum katika jimbo la Monduli wiki ijayo kuzungumzia
tatizo la ardhi.Semina iliyoandaliwa na Mh Lowassa itawashirikisha
viongozi wote wa wilaya hiyo pamoja na wakuu wa kimila.Akizungumzia
suala la ardhi mzee John Keen alisema mtu anayeuza ardhi anauza utajiri
na kununua umasikini |
No comments:
Post a Comment