Tuesday, 7 October 2014

MH. LOWASSA AMKARIBISHA MONDULI BALOZI WA JAPAN NCHINI TANZANIA

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimkaribisha wilayani Monduli Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada wakati alipowasili wilayani humo jana Jumapili Septemba 28,2014 kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na nchi hiyo.Balozi huyo aliahidi kusaidia vifaa vya kisasa katika hospitali mpya ya kisasa inayojengwa wilayani humo.

Meneja wa Hoteli ya Emanyata mjini Monduli,Bi. Neema (kushoto) akiwa na Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada hotelini hapo.Pembeni kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli.
Meneja wa Hoteli ya Emanyata mjini Monduli,Bi. Neema (kushoto) akimkaribisha Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada hotelini hapo.Pembeni kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli.       
 Tembelea jimboni kwake Monduli kupitia http://elowassa.com/monduli_swahili.php


No comments:

Post a Comment